LULU AWAPA MAKAVU WANAOSIFIA UZURI WA MTU KWA KUMPONDA MWINGINE


“Niongee kidogo kuhusu hili kwa wanawake na wanaume....hivi kuna baadhi ya Watu mnashindwa kabisa kumsifia mtu bila kuponda wengine....!?? Au kupenda mtu bila kuchukia wengine...!?Kwa ufupi tu iko hivi....Kila mwanamke duniani ana uzuri wake na a ana kitu ambacho mwanamke mwingine hana,hata wanaume pia...!

Sasa kuna watu fulani hawawezi kabisa kumsifia mtu bila kumponda mwingine, inafurahisha sana kutaka kulazimisha kuwa Mungu.....hivi unafikiri Mungu alikuwa hayuko sawa kufanya wanawake wawe wengi tena wengi zaidi ya wanaume, we fikiria tu na utulize akili yako ya kipuuzi.....!!!Hapa ni duniani ukiona unataka kuwa pekeyako pekeyako au kusifia mtu kwa kuponda wengine ni bora ufanye maombi  Mungu akupeleke/au ampeleke mtu wako sayari ya tofauti na dunia kama Jupiter huko auu Pluto mana duniani ndo tumeshajazwa hvyo.
Maneno yamekuwa mengi Lakini maana yangu ni hii hakuna Haja ya kumsifia mtu kwa kuponda wengine au kumpenda mtu kwa kuchukia wengine”.-Lulu alimaliza

Tafakari chukua hatua!!!
LULU AWAPA MAKAVU WANAOSIFIA UZURI WA MTU KWA KUMPONDA MWINGINE LULU AWAPA MAKAVU WANAOSIFIA UZURI WA MTU KWA KUMPONDA MWINGINE Reviewed by Unknown on 3:23:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.