Siku ya jana asubuhi kulikuwa na ishu ya mitandao ya Facebook na Instagram kupata matatizo, ikatia hofu kwa baadhi ya watumiaji wakiwa wanahisi kwamba labda tayari account zao zimevamiwa na hackers kama ambavyo imekuwa ikitokea mara nyingi.
Wapo waliodhani kwamba sababu huenda ni ishu ya network ambayo tumekuwa tukiiona mara nyingi, taarifa rasmi iliyoripotiwa jana January 27 na wataalamu wanaoendesha mitandao hiyo ni kwamba lilijitokeza tatizo lililofanya mitandao hiyo kukaa offline kwa kama dakika 40 hivi.
Tatizo hilo lilitokana na ishu ya wataalamu hao kufanya mabadiliko katika mpangilio wa system za mitandao hiyo, kukatokea matatizo ambayo walishughulikia ndani ya muda mfupi na kila kitu kikarudi sawasawa.
“Earlier this evening many people had trouble accessing Facebook and Instagram… This was not the result of a third-party attack but instead occurred after we introduced a change that affected our configuration systems. We moved quickly to fix the problem, and both services are back to 100% for everyone”—alinukuliwa msemaji wa Kampuni inayosimamia mitandao hiyo.
Kama ulipata tatizo lolote kwenye account zako kwenye Instagram na Facebook hii ni taarifa rasmi kutoka kwa wamiliki wa mitandao hiyo.
credit;udaku special
Huenda Ulipata Tatizo Jana Kwenye Account yako ya FACEBOOK, INSTAGRAM? Hiki ndicho Kilichotokea
Reviewed by Unknown
on
2:05:00 AM
Rating: