KAJALA AFUNGUKA==>> NIPO TAYARI KUGHARAMIA HARUSI YA WOLPER NA MANAIKI

KAJALA MASANJA (KATIKATI) AKIWA NA JACQUELINE WOLPER (KUSHOTO).

MWANADADA anayefanya vizuri kunako soko la filamu za Kibongo, Kajala Masanja ‘Kay’ ameweka wazi kuwa yuko tayari kugharamia sherehe ya harusi ya Manaiki Sanga na Jacqueline Wolper Massawe kama mambo yataenda sawa.


Akipiga stori na Uwazi, Kajala alisema kutokana na ukaribu alionao kwa watu hao basi mambo yote yanayohusiana na sherehe yatakuwa chini yake kwa maana ya gharama zote na kikubwa ni kuwaombea tu maana ni muda mrefu sana Manaiki alikuwa na ndoto za kumuoa Wolper.

Jacqueline Wolper akiwa na Manaiki “Ukiachana na Wolper kuwa rafiki yangu, Manaiki ni ‘staff’ kwenye ofisi yangu na nimefanya naye kazi nyingi sana kabla hata sijafungua kampuni yangu hivyo nitasimamia sherehe yao mwanzo mpaka mwisho kwa gharama zozote zile, naomba Mungu amsaidie Manaiki barua yake ya posa ikubaliwe,” alisema Kajala.
Kwa upande wake Manaiki alisema;

“Namshukuru Kajala kwani ana moyo wa pekee na furaha yangu itakuwa kubwa pale nikiwa nimekubaliwa rasmi kumuoa Wolper kwa sababu ni mtu ambaye nimemfahamu kwa muda mrefu na hata yeye pia.”
KAJALA AFUNGUKA==>> NIPO TAYARI KUGHARAMIA HARUSI YA WOLPER NA MANAIKI KAJALA AFUNGUKA==>> NIPO TAYARI KUGHARAMIA HARUSI YA WOLPER NA MANAIKI Reviewed by Unknown on 6:13:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.