Kila mtu ana haki na uhuru wa kuandika au kuweka chochote kile anachojisikia kwenye akaunti zake za kwenye mitandao ya kijamii “social networks” ilimradi asivunje sheria za mitandao hiyo.Lakini uhuru na haki hiyo kwa watu mashughuri hali huwa tofauti kabisa unabisha?? Muulize Davido.
Turudi Kwenye Mada
Leo mrembo na mwigizaji wa filamu hapa bongo, Jackline Massawe “Wolper” kupitia ukurasa wake wa kwenye mtandao wa INSTAGRAM aliweka picha hiyo hapo juu ya filamu ya NDOA YANGU ambayo “alicheza” pamoja na marehemu Steven Kanumba na kuandika neno “DAIMAAAA”
Katika hali isiyokuwa ya kawaida watu wengi walionyesha kupatwa na simamzi na majinzi mazito na wengine kuandika wametokwa na machozi mara baadaya kuona picha hii.
Japo kuwa naamini mwanadada Wolper aliweka picha hii kwania njema na wengi walimtakia kheri marehemu Kanumba na kumsifia kwa kile alichokifanya enzi za uhai wake lakini wapo baadhi ya watu walilamika kuwa picha hii imewarudishia machungu na hivyo kumshushia lawama Wolper alieiweka.
Sijui wewe umelichukuliaje hii.
WOLPER AAMSHA SIMANZI KWA MASHABIKI WAKE!!!
Reviewed by Unknown
on
12:05:00 AM
Rating: