HABARI MBAYA KWA DIAMOND>>>MFANYABIAHSARA MKUBWA NCHINI UGANDA AMUITA DIAMOND "SHOGA" ETI KISA NI ZARI

HII ni ‘bad news’ kwa staa namba moja wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’. Mfanyabiashara maarufu nchini Uganda anayefahamika kwa jina la King Lawrence, ameibuka na kumuita nyota huyo shoga, Ijumaa linakupa habari hii.

Staa namba moja wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na Zarinah Hassan ‘Zari’.

ISHU ILIPOIBUKIA
King ambaye ana makazi yake pia nchini Afrika Kusini, amedaiwa kutoa kauli hiyo juzi, Jumatano kupitia mtandao wa Facebook akionesha kukerwa na kitendo cha staa wa muziki Uganda, Zarinah Hassan ‘Zari’ kuangukia katika penzi la Diamond.

ATUMIA GIA YA WATOTO
Awali, King ambaye imeelezwa alikuwa na urafiki na dereva wa aliyekuwa mume wa Zari, Ivan Semwanga, alianza kwa kumchokonoa Diamond kwa gia ya kujifanya anawatetea watoto wa Zari ambapo alitupia picha ya Zari akiwa na Diamond mtandaoni ikiwa na ujumbe wenye kejeli na jeuri ya fedha.

UJUMBE ULIVYOSOMEKA
“As a concerned uncle, Im offering Zari’s tomboy Diamond Dola 40,000 so as to leave the old mom of three to take care of her kids. The young boys miss their mom. Please Diamond do it for the kids.”
(Nikiwa kama mjomba, ninampa jikedume wa Zari, Diamond, Dola 40, 000 (Sh. Mil 66) ili amuache mama wa watoto watatu (Zari) awalee vizuri watoto wake. Watoto wanammisi mama yao.”

Diamond Platnumz na Zari wakidendeka.


ABADILISHA GIA
Kuonesha ana mpango mchafu wa kumchafua Diamond ambaye anaipeperusha vyema bendera ya Afrika kimuziki, badala ya ishu ya watoto, alibadili upepo na kujinadi eti yeye ndiye wa kwanza kutembea na Zari.
Pasipo kueleweka kusudi lake, alimpiga dongo Diamond ambaye usiku wa kuamkia leo alipewa heshima ya kipekee kutumbuiza kwenye Tuzo za Wanamichezo Bora zilizoandaliwa na Shirikisho la Afrika (Caf) nchini Nigeria.

HEBU MSIKIE
“Kwa nini utembee na Diamond shoga? Sijui kama anajua kwamba mimi ndiyo wa kwanza kutembea na wewe (Zari),” aliandika katika mtandao wa Facebook.

AZIDI KUTAPATAPA
Kama hiyo haitoshi, kupitia mtandao wa Facebook, King alitupia mawasiliano yake ya zamani na Zari akidai alikuwa akimuomba fedha.

DIAMOND ANASEMAJE?
Hadi tunakwenda mitamboni, jitihada za kumpata Diamond ili aweze kujibu tuhuma hizo hazikuzaa matunda huenda ni kutokana na ubize aliokuwa nao katika maandalizi ya shoo hiyo kubwa Afrika, simu yake iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi, hakujibu.

King Lawrence.

ZARI AMSAFISHA DIAMOND
Kupitia mtandao huo, Zari naye aliibuka na kumtetea Diamond akimwambia King ana chuki binafsi kwani hapendi kumuona akiwa na furaha.

“Hatuna muda wa kukujadili, unafikiri Diamond anaweza kuwa shoga? Unafikiri anaweza kubishana na wewe? Kweli nimeamini, watu wakikuona una furaha, wanaanza kukuchukia,” alijibu Zari maneno hayo ambayo pia ameyaweka katika akaunti yake ya mtandao wa Instagram.

DIAMOND NI SHOGA?

Kutokana na madai hayo ya King, baadhi ya wadau wakubwa wa muziki Bongo walikanusha vikali madai hayo kwa kudai jamaa huyo ana lengo la kumchafua Diamond kwa kuwa kwa sasa anafanya vizuri Afrika nzima.
“Hana lolote huyo King, anatafuta kiki za kipuuzi, atamuitaje Diamond shoga? Amewahi kumuona akifanya vitendo hivyo? Wivu tu wa maendeleo, aache Diamond na Zari wafanye yao, apeperushe muziki wetu nje ya Afrika,” alisema mdau mmoja ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini.

KING ANATESWA NA WIVU?
Licha ya awali King kutoonesha kwamba aliwahi kutembea na Zari, katika maelezo yake ya pili yameonesha dhahiri kwamba anasumbuliwa na wivu wa mapenzi kutokana na kujinadi kuwa yeye alikuwa wa kwanza kutembea na Zari.
“We huoni ameanza kwa kujifanya anawatetea watoto, mara akajifanya rafiki wa dereva wa Ivan mara tena amegeuka anadai alikuwa wa kwanza kutembea na Zari hana lolote wivu tu unamsumbua atakuwa alimtaka mtoto mzuri akamchomolea,” aliandika mdau mmoja katika mtandao wa Instagram.

KING NI NANI?
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, jamaa huyo ni mfanyabiashara maarufu nchini Uganda na Afrika Kusini na amekuwa akijinasibu kuwa na uhusiano na mastaa mbalimbali wa Uganda akiwemo mwanamuziki Julia Kanyomozi.
HABARI MBAYA KWA DIAMOND>>>MFANYABIAHSARA MKUBWA NCHINI UGANDA AMUITA DIAMOND "SHOGA" ETI KISA NI ZARI HABARI MBAYA KWA DIAMOND>>>MFANYABIAHSARA MKUBWA NCHINI UGANDA AMUITA DIAMOND "SHOGA" ETI KISA NI ZARI Reviewed by Unknown on 10:42:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.