MAKUBWA YAIBUKA>>> MSANII WOLPER ATIBUA UCHUMBA WA "NEY WA MITEGO"





Mwigizaji wa filamu Bongo Jacqueline Wolper.

Stori: Musa mateja
KIMENUKA! Mwigizaji Jacqueline Wolper ameibua tafrani la aina yake kwa Mbongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ baada ya kumtumia meseji iliyomtia shaka mpenzi wa staa huyo, Siwema.

Tukio hilo lilitokea juzikati nyumbani kwa Nay wa Mitego, Kimara- Korogwe jijini Dar ambapo ilisemekana Wolper alituma SMS iliyokuwa ikiuliza muafaka wa jambo fulani ndipo Siwema akaja juu na kuanza kumcharukia bebi wake huyo.

Mbongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ akiwa na mpenzi wake Siwema.

Alipoulizwa Nay wa Mitego kuhusiana na ugomvi huo, alifunguka:
“Wolper ni rafiki yangu kitambo, ni mtu wangu tunayeelewana kupita maelezo, hivyo juzikati nilikuwa nikichati naye juu ya kutaka kumshirikisha kwenye video ya wimbo wangu mpya wa Akadumba, Siwema dizaini kama alimaindi kuona nawasiliana naye lakini nilimuelewesha na kila kitu kipo sawa.”
MAKUBWA YAIBUKA>>> MSANII WOLPER ATIBUA UCHUMBA WA "NEY WA MITEGO" MAKUBWA YAIBUKA>>> MSANII WOLPER ATIBUA UCHUMBA WA "NEY WA MITEGO" Reviewed by Unknown on 1:41:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.