Akizungumza katika wodi ya wazazi katika Hospitali hiyo Muuguzi wa zamu, Naabu Geraruma, amesema kuwa mwanamke huyo amefanikwa kujifungua Januari 5, 2015 usiku wa saa saba kwa njia ya operesheni ambapo watoto hao wenye jinsi ya kike wamezaliwa wakiwa na uzito wa kilo 4.6.
Amesema tukio hilo ni la kwanza kutokea katika Hospitali hiyo na kwamba hali ya mwanamke huyo na watoto zinaendelea vema na taratibu za kumpeleka katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mwanza Bugando zimekamika.
Taarifa kutoka jijini Mwanza na kuthibitishwa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasmali Watu wa hospitali hiyo, Leah Kagine, zinasema tayari mwanamke huyo na watoto wamefikishwa katika hospitali hiyo kwa ajili ya matibabu na uchunguzi zaidi.
MAAJABU>>> MAMA AJIFUNGUA WATOTO MAPACHA WALIOUNGANA KATIKA MAENEO YA KIFUA HUKO MKOANI MARA
Reviewed by Unknown
on
9:58:00 PM
Rating: