KASHFA YA KURUDIA MAVAZI KWENYE VIDEO>>>OMMY DIMPOZ AWAPA MAKAVU WALIOMPONDA KUWA ANARUDIA SUTI ZA KUVAA
Fid Q aliwahi kusema ‘uspastaa ni mzigo wa miiba’ na pengine huu wa Ommy Dimpoz umekuwa mzito kiasi cha kuamua kuzungumza.
Apparently wabongo wanahisi suti aliyoivaa kwenye shooting ya wimbo alioshirikishwa na Avril, ‘Hello Baby’, ndio ile ile aliyoivaa kwenye video ya wimbo wa Diamond f/ Iyanya’ Bum Bum.
Kuthibitisha kuwa hizo ni suti mbili tofauti, Ommy ameweka picha mbili tofauti zilizounganishwa akiwa amevaa suti za blue zinazofanana muundo lakini zinazotofautiana ung’aavu wake.
“Jibu kwa wanaosema nairudia kuivaa sana suti yangu,” ameandika Ommy kwenye Instagram.
“Je unavyoona hapo hiyo ni suti moja au mbili ambazo zimefanana vifungo? Hizo ni picha ambazo hazija editiwa, swali langu kwa wataalam wa kuchambua mambo mafashonista wa Instagram hivi ukiwa supastaa au kioo cha jamii haurusiwi kurudia nguo?,” amehoji.
“Jamani nguo yangu lakini napangiwa masharti eti nisivae sana kisa Ommy Dimpoz, kheee makubwaa! Yaani nilichogundua kumbe hata Obama ana suti yake fulani hivi amazing nyeusi anaivaa kila siku kumbe habadilishi? Mwanzo mlisema ‘ooh mshamba kaja na treni kavaa yeboyebo; haya sasa hivi tena ‘ooh mshamba anarudia suti’ khee sasa nifanyeje jamani.”
KASHFA YA KURUDIA MAVAZI KWENYE VIDEO>>>OMMY DIMPOZ AWAPA MAKAVU WALIOMPONDA KUWA ANARUDIA SUTI ZA KUVAA
Reviewed by Unknown
on
9:29:00 PM
Rating: