BREAKING NEWS: WATU NANE AKIWEMO MAMA MJAMZITO WAMENUSURIKA KIFO BAADA YA KUNYWA MAZIWA YENYE SUMU SINGIDA

Watu nane wa familia tatu akiwemo mama mjamzito wa kijiji cha nkuhi wilayani ikungi,wamenusurika kufa baada ya kunywa maziwa yanayo sadikiwa kuwa na sumu.
Wakieleza kwa shida akiwemo aliye wauzia maziwa hayo huku wakiwa wamelazwa katika hospitali teule ya masister wa malikia wa ulimwengu iliyopo katika kijiji cha puma ,wamesema baada ya kunywa maziwa hayo walianza kuumwa na tumbo huku wakiharisha na kutapika kwa mfululizo
Mganga mfawidhi wa hospitali teule ya masister wa malikia wa ulimwengu Daktari Corbinian Nyenyembe,amesema wamepokea wagonjwa wanao sadikiwa kunya sumu wa familia tatu akiwemo mama mmoja ambaye ni mjamzito,watu wakubwa watatu na watoto wanne ambao ni wanafunzi wa shule ya msingi mkiwa wilayani ikungi,baadhi yao wakiwa na halimbaya na wanaendelea na matibabu.

Bwana Jeremia Saudi ni baba wa watoto watatu walio kunywa maziwa na wamelazwa katika hospitali hiyo ,amesema wamebaini kuwa maziwa hayo yanaweza kuwa na sumu baada ya kaka yake kuyaonja na kukuta siyo kama maziwa mengine.
BREAKING NEWS: WATU NANE AKIWEMO MAMA MJAMZITO WAMENUSURIKA KIFO BAADA YA KUNYWA MAZIWA YENYE SUMU SINGIDA BREAKING NEWS: WATU NANE AKIWEMO MAMA MJAMZITO WAMENUSURIKA KIFO BAADA YA KUNYWA MAZIWA YENYE SUMU SINGIDA Reviewed by Unknown on 9:15:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.