Diamond na Davido wana beef? Hili ni swali ambalo watu wengi bado hawajapata jibu lake hasa baada ya wiki hii Davido kutweet maneno yaliyohisiwa kuwa yanamlenga Diamond.
Akizungumza kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM Ijumaa hii, meneja wa Diamond, Babu Tale amesema Diamond na Davido sio washkaji ila wana mahusiano ya kibiashara tu.
“Hakuna vita mimi na menejimenti ya Davido, Tunaongea,” amesema Tale.
“Hapa ninaweza nikakuonesha meseji za mimi na Kamala ambaye ni meneja wa Davido. Nikinukuu maneno ya Kamala kwangu ile meseji ambayo Davido aliposti ya kwanza hakuwa anamface Diamond according to Kamala. Akaniambia mbona ‘watanzania wameelewa vibaya’ nikamwambia ‘tuliache hili limepita na limeshatokea hatuwezi kuwaambia bana Davido hajaongea hivi kwa maana hii, tutafute njia nyingine ambayo Davido anaweza akasehewa na Watanzania,” ameongeza Tale.
“Lakini sitaki kuamini kama Davido na Diamond wana vita. Juzi Davido alikuwa anaposti vitu vyake sio kwa sababu ya Diamond. Watanzania wote washaanza kusema ‘oooh Davido ashaanza kumtukana Diamond’.
Nikwambie kitu kimoja Diamond hata baada ya kufanya ile video huwaga hawachati, Diamond akimtaka Davido ataniambia mimi au atamwambia Salam au Kamala.”
BIFU LA DIAMOND NA DAVIDO SASA LAFIKA MWISHO>>>BABU TALE MENEJA WA DIAMOND PLATNUM AFUNGUKA MAZITO
Reviewed by Unknown
on
9:07:00 PM
Rating: