Rais Magufuli Amwaga Mabilioni Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu..Shirikisho la Wanafunzi wa vyuo vikuu Tanzania Wasema Haya


Shilingi billion 473 zimetengwa kwa ajili ya kutoa mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu nchini kwa mwaka huu ikilinganishwa na Shilingi bilioni 341 zilizotolewa mwaka jana ikiwa ni ongezeko la Tsh. bilioni 132 katika bajeti ya mwaka huu.

Hayo yalisemwa jana jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa shirikisho la wanafunzi wa vyuo vikuu Tanzania(Tahliso) bwn. Nzilanyingi John alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuaandaa mdahalo kujadili hotuba ya Rais Dkt. John Magufuli aliyoisoma Dodoma wakati wa ufunguzi wa bunge la kumi na moja .

Alisema kuwa kwa kipindi kifupi kumekuwa na mabadiliko ya haraka yaliyotokea katika sekta ya elimu nchini kwa mwaka huu kwani kuna ongezeko la zaidi ya wanafunzi 1800 waliopata mkopo ikilinganishwa na mwaka uliopita ambapo ni wanafuzi 34128 pekee ndio waliofanikiwa kupata mkopo.

“Mpaka sasa jumla ya wanafunzi 51,675 wa mwaka wa kwanza wamepata mkopo na lengo ni kufikia 53,032, pia jumla ya wanafunzi 91 wa shahada ya uzamili na wanafunzi 113 wanaosoma vyuo vya nje tayari wamepata mkopo” alisema John.

Aliongeza kuwa katika kipindi kifupi kijacho bodi ya mikopo imehakikisha kutoa mikopo kwa wanafunzi zaidi ya elfu moja wanaochukua Diploma maalumu ya ualimu Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na hivyo kukamilisha adhma yao ya kutoa mikopo kwa wanafunzi 53,032.

Aidha shirikisho hilo ambalo ni umoja wa viongozi wa serikali za wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini umeandaa mdahalo wenye lengo la kutoa fursa kwa watanzania wengi kujadili hotuba hiyo na namna rais alivyoanza kutekeleza majukumu yake katika nafasi hiyo.

Mdahalo huo utafanyika jijini Dar es Salaam tarehe 13 mwezi huu katika ukumbi wa Nkurumah na wazungumzaji wakuu katika mdahalo ni Mtaalamu mbobevu wa uchumi kutoka chuo kikuu cha Mzumbe Prof.Honest Ngowi, Dkt. John Lingu kutoka Idara ya Sayansi ya Siasa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mwanadiplomasia Christopher Liundi.
Rais Magufuli Amwaga Mabilioni Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu..Shirikisho la Wanafunzi wa vyuo vikuu Tanzania Wasema Haya Rais Magufuli Amwaga Mabilioni Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu..Shirikisho la Wanafunzi wa vyuo vikuu Tanzania Wasema Haya Reviewed by Unknown on 10:50:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.