MO MUSIC MATATANI..!! ASHIKILIWA NA POLISI KWA UTAPELI WA MAMILIONI YA FEDHA



NI SOO! Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Moshi Katemi maarufu kama Mo Music, ametiwa mbaroni mjini Dodoma kwa madai ya utapeli wa mamilioni ya shilingi ya kigogo anayetajwa kwa jina moja la Barthazar, ambaye ni mhadhiri wa Chuo cha Mipango cha mjini humo.

Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika, ishu hiyo ilitokea wiki iliyopita baada ya kuhusishwa na msichana aitwaye Joyce Ngerangera ambaye awali alikuwa ni mpenzi wa mhadhiri huyo.

Inadaiwa kuwa Mo Music alikamatwa wakati akitoka nje ya Studio ya Radio Free Africa jijini Dar es Salaam kwenye mahojiano, ambapo makachero waliotumwa kutoka Dodoma, walimtaka aende Kituo cha Polisi Oysterbay.

“Walikwenda naye kituoni na baadaye akasafirishwa kwenda Dodoma ambako alitoka kwa dhamana, kesi yake ilihusiana na kupewa pesa na Joyce ambaye alikuwa akizichuma kwa Barthazar, jamaa alichukia baada ya kubaini kuwa licha ya kuchukuliwa fedha zake, pia Mo alikuwa akitembea na demu huyo,” kilisema chanzo hicho.

Gazeti hili lilimtafuta Mo Music ambaye alifunguka kuwa ni kweli alikamatwa kwa ishu hiyo, lakini akasema haelewi lolote zaidi ya ukweli kuwa kwa kipindi kifupi, aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Joyce.

“Huyo demu nilishaachana naye kitambo tu, sasa kilichopo ni kwamba huyu mwanamke alimchezea mchezo jamaa, siku moja wakati wakifanya yao kwenye gari, demu aliwaita watu wakajifanya polisi, wakawapiga picha na kumwambia huyo mwanaume awape pesa la sivyo watamchafua, ikabidi awape milioni mbili.

“Sasa kila baada ya muda alikuwa akichukua simu ya mtu yeyote na kujifanya ndo wale maaskari awape pesa, naye anatuma, siku moja alichukua simu yangu akasema kuna mtu atamtumia pesa maana simu yake imezima chaji, ikatumwa laki na nusu, mimi sijui kama ni dili anacheza, cha ajabu baada ya kushtukia hiyo ishu, jamaa anadai mimi ndiyo nahusika na mchezo mzima hivyo ananidai milioni thelathini na nne alizotapeliwa wakati sihusiki kabisa,” aliongeza Mo Music.

Kwa upande wake Joyce alikiri kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Barthazar uliodumu kwa mwaka mmoja kabla ya kushindwana na yeye kuanza na Mo Music.

“Kinachomsumbua ni wivu kisa nimeachana naye, kama ni kesi angetakiwa adili na mimi, siyo Mo Music, anamuonea tu, hahusiki hata kidogo kwenye hiyo ishu,” alisema.
Barthazar alipotafutwa, alisema hawezi kuiongelea kesi hiyo iliyofunguliwa jalada namba DOM/IR/6365/2015 KUJIPATIA PESA KWA NJIA YA UDANGANYIFU, kwa kile alichosema kuwa kesi hiyo imefunguliwa na Jamhuri hivyo hawezi kuiongelea, labda kama ataulizwa msanii huyo.
 
MO MUSIC MATATANI..!! ASHIKILIWA NA POLISI KWA UTAPELI WA MAMILIONI YA FEDHA MO MUSIC MATATANI..!! ASHIKILIWA NA POLISI KWA UTAPELI WA MAMILIONI YA FEDHA Reviewed by Unknown on 1:08:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.