SHILOLE AWAPA MAKAMU WANAOMTUKANA>>>HIKI NDICHO ALICHOSEMA

Katika hali isiyokuwa ya kawaidi msanii shilole amefunguka na kutoa ya moyoni kuhusu mashabiki wanao wa-follow wasanii katika mitandao ya kijamii kutokana na baadhi ya mashabiki kutumia mitandao hiyo kuwachafua wasanii hao kutokana na kuwakejeli hadi kufikia hatua ya kuwatukana hadharani kupitia mitandao hiyo.



Kupitia A/C yake ya Instagram shilole ameposti ujumbe huu kuhusu baadhi ya mashabiki wenye tabia ya kuwakashifu wasanii kupitia mitandao hiyo.



“Hivi mashabiki zangu niwaulize swali!?? Hivi unapom-follow mtu ili uwe unamtukana Tuuùu kila akipost picha yake?? Au unam-follow ili upate kuona anafanya nini?? Katika kazi , kiukweli mimi nakelekwa sana na baadhi ya mashabiki zangu naona kama wakuwa sio wazalendo kabisaaà kila ufanyalo yeye kwake anaona baya tu acheni roho za kwanini! Ukiona mtu kafanya vizuri msifie tu na kama unaona hajakufurahisha mwambie tu kwa uzuri kwani matusi hayajengi! “

Shilole aliendelea;

“Mimi kama msanii nategemea maoni yenu mazuri na sio matusi yenu tujaribu kuiga mifano kwa nchi za wenzetu wanapenda wasanii wao na kuwajali lakin huku sisi kutwa mnatuchamba loh! Na sisi pia wakati mwingine tunaumia na matusi yenu yasio na maana! But ukitaka kunitukna uwe na tusi jipya la 2015 yani unitukane huku unanipa PESA. Nawapenda sana team saport wasanii wa home kuweni na J2 njema”-Shilole alimaliza.


Ujumbe umefika, tubadilike jamani
SHILOLE AWAPA MAKAMU WANAOMTUKANA>>>HIKI NDICHO ALICHOSEMA SHILOLE AWAPA MAKAMU WANAOMTUKANA>>>HIKI NDICHO ALICHOSEMA Reviewed by Unknown on 1:18:00 PM Rating: 5
Powered by Blogger.