MREMBO HUDDAH AMNASA MKONGO WA WWOLPER, HUU APA USHAHIDI WAKIWA KWENYE POZI LA KIMAHABA


Mfanyabiashara wa Kongo, Mwami Radjabu akipozi kimahaba na mwanamitindo wa nchini Kenya, Huddah Monroe.DUH! Kweli fedha mwanaharamu. Yule mfanyabiashara aliyewatikisa mastaa wa Bongo kwa kuwa nao kimapenzi, Mwami Radjabu raia wa Kongo hivi sasa amehamia kwa mwanamitindo wa nchini Kenya, Huddah Monroe. 
Mkongo huyo ambaye alikuwa na uhusiano na msanii wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper hivi karibuni picha zake akiwa na Huddah kimahaba zilinaswa ambapo chanzo kilieleza kwamba wawili hao ni wapenzi na kwa sasa Mkongo huyo yupo Kenya wanaponda raha.“Mh, mastaa wa kike wa Bongo waliokuwa wanamshobokea Mkongo wakome kwa sababu sasa hivi yupo na Huddah na amewaacha solemba na anasema hataki kuwasikia,” kilisema chanzo makini kilicho karibu na Mkongo huyo.

Mwami Radjabu na Huddah Monroe wakila ujana. Baada ya kuzinyaka habari hizi, gazeti hili lilimtafuta Mkongo ambapo alikuwa na haya ya kusema;
“Ni kweli ni muda mrefu niko Kenya na Huddah ndiye mpenzi wangu kwa sasa naomba hao mademu wa Bongo wanikome kabisa kwani wamezidi, nitakuja naye huko Dar Januari 10, mwaka huu kuhusu Wolper atabaki kuwa rafiki yangu wa kawaida tu.”
MREMBO HUDDAH AMNASA MKONGO WA WWOLPER, HUU APA USHAHIDI WAKIWA KWENYE POZI LA KIMAHABA MREMBO HUDDAH AMNASA MKONGO WA WWOLPER, HUU APA USHAHIDI WAKIWA KWENYE POZI LA KIMAHABA Reviewed by Unknown on 1:12:00 AM Rating: 5
Powered by Blogger.