Waswahili wanasema ukweli unauma na wakati mwingine pamoja na msemwa ukweli kuwa kipenzi cha Mungu, huonekana mwenye dharau.
Hiki ndicho kilimkuta Diamond Platnumz
kwenye ziara yake nchini Rwanda. Wakati akiongea na waandishi wa habari
mjini Kigali, Diamond alidai kuwa wasanii wa Rwanda hawajitangazi
kimataifa.
Kauli hiyo haikuwaingia vyema baadhi ya
wasanii wa Rwanda akiwemo Jay Polly aliyekuwa mmoja wa wale
waliomsindikiza kwenye show yake jijini humo.
Mshindi huyo wa msimu wa nne wa shindano
la muziki la PGGSS, alidai ni ukosefu wa heshima msanii mgeni kudharau
muziki wa Rwanda ambao alidai upo mahala pazuri.
“Kuna msanii mgeni atakayetumbuiza hapa
leo. Nilisikia kwenye habari akidai kuwa wasanii wa Rwanda hawajui
wanachokifanya,” alisema msanii huyo mbele ya maelfu ya wapenzi wa
muziki mjini Kigali waliokuwa wamekusanyika kwenye uwanja wa Amahoro.
“Hilo lina ukweli gani ? Mnakubaliana
naye? Inawezekanaje kuwa hatujui?” “Muziki wa Rwanda utaendelea kuwepo.
Tutaupeleka kwenye hatua tunayotaka lakini kwa kuona tulipo sasa, hakuna
mwenye haki ya kusema hatujui tunachokifanya,” aliongeza rapper huyo.
Hata hivyo gazeti la New Times la Rwanda
limedai kuwa show aliyotumbuiza Diamond ilithibitisha wazi utofauti
wake na wasanii wa Rwanda.
“Ni wazi kuwa show ya Diamond ilisimama
ukilinginisha na zile za mwanzo,” mmoja wa mashabiki waliohudhuria show
hiyo aitwaye Nina Uwase aliliambia gazeti hilo.
“Kiukweli, baadhi ya wasanii iliwabidi
waumeze ukweli huo unaouma na kuungana na umati wa watu kumshangilia
Diamond wakati alipokuwa akidondosha show ya nguvu ambayo huenda
ilimfanya Jay Polly kufikiria mara mbili kauli yake aliyoitoa awali,”
limeandika gazeti hilo.
DIMOND AWACHUKIZA WASANII WA RWANDA>>>WAAMUA KUMTOLEA MANENO MACHAFU, HIKI NDICHO KILICHOWAKERA
Reviewed by
Unknown
on
10:35:00 AM
Rating:
5